• HABARI MPYA

  Friday, April 20, 2018

  NANE BORA LIGI KUU YA WANAWAKE KUENDELEA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Wanawake Hatua ya Nane Bora inatarajia kuendelea Wikiendi hii.
  Jumamosi Aprili 21,2018 zitachezwa mechi Tatu na mchezo mmoja utachezwa Jumapili Aprili 22,2018.
  Jumamosi Kwenye Uwanja wa Karume Evergreen watawakaribisha Alliance , wakati kwenye Uwanja wa Mbweni JKT Quenns watakuwa wenyeji wa Simba Queens nayo Kigoma Sisterz ikiwa Uwanja wa Tanganyika kuwaalika Baobab.
  Mchezo wa Panama dhidi ya Mlandizi Queens wenyewe utachezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Samora Iringa.
  Ligi hiyo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake iliyokuwa na mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake dhidi ya Zambia.
  Katika hatua nyingine Wadhamini wa Ligi hiyo ya Wanawake kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Bia yake ya Serengeti Premium Lite,imekabidhi mavazi rasmi kwa timu zote.
  Meneja Masoko wa Serengeti Anitha Msangi amesema Serengeti inaamini kuwa kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake wanachangia kuleta maendeleo ya Mpira wa Wanawake.
  Amesema Mashabiki wanayo nafasi kubwa katika maendeleo ya Mpira wa Wanawake na kuwataka waweze kujitokeza kuunga mkono Ligi Kuu ya Wanawake pamoja na kuziunga mkono timu za Wanawake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NANE BORA LIGI KUU YA WANAWAKE KUENDELEA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top