• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 30, 2018

  SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA

  Winga wa Simba SC, Shiza Kichuya (kulia) akiuchukua mpira kiufundi dhidi ya kiungo wa Yanga SC, Juma Mahadhi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Simba ilishinda 1-0 
  Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi akipasua katikati ya mabeki wa Yanga, Kelvin Yondan (kushoto) na Andrew Vincent 'Dante' (kulia)
  Mawinga, Shiza Kichuya wa Simba SC (kushoto) na Yussuf Mhiulu wa Yanga (kulia) wakigombea mpira 
  Mfungaji wa bao pekee la Simba jana, Erasto Nyoni (katikati) akijivuta kupiga mpira dhidi ya mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa. Kushoto na refa msaidizi namba mbili, Mohammed Mkono wa Tanga 
  Kiungo wa Simba, Jonas Mkude akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Yanga, Ibrahim Ajib
  Ibrahim Ajib wa Yanga akimtoka mshambuliaji Mghana wa Simba, Nicholaus Gyan anayetumika kama beki kwa sasa 
  Obrey Chirwa akimtoka Erasto Nyoni katika mchezo wa jana
  Nahodha wa Simba, John Bocco akimtoka Ibrahim Ajib jana
  Kikosi cha Simba SC kabla ya mchezo wa jana
  Kikosi cha Yanga SC kabla ya mchezo wa jana 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top