• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 26, 2018

  MZUNGU WA AZAM ASIMAMISHWA LIGI KUU KWA KUMTUSI REFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mromania wa Azam FC, Aristica Cioba amesimamishwa hadi suala lake la kumtukuna Mwamuzi baada ya mechi kumalizika litakaposikilishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi kutokana na makosa anayodaiwa kuyafanya katika mechi namba 194 dhidi ya Njombe Mji.
  Kabla ya kumtukana Mwamuzi, Kocha huyo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) kwa kupinga maamuzi kwa maneno na vitendo katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 15, 2018 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MZUNGU WA AZAM ASIMAMISHWA LIGI KUU KWA KUMTUSI REFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top