• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 28, 2018

  MADAKTARI WA WANAMICHEZO WAZUIWA KUFANYA UCHAGUZI HADI...

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Wanamichezo (TASMA), imehairisha uchaguzi wa Chama hicho uliokuwa ufanyike kesho Jumapili Aprili 29, 2018 hadi hapo itakapotangazwa tena.
  Kamati hiyo ya uchaguzi wa TASMA chini ya Mwenyekiti wake, Leslie Liunda imesema sababu kubwa ya kuhairishwa kwa uchaguzi huo ni kamati ya utendaji kushindwa kutekeleza mahitaji ya msingi ya maandalizi ya uchaguzi husika.
  Moja kati ya yale yaliyoshindwa kutekelezeka ni pamoja na kukosekana kwa fedha ya kuendeshea uchaguzi huo.
  Kutokana na sababu hizo Kamati imehairisha uchaguzi mpaka pale Kamati ya Utendaji ya TASMA na kamati ya uchaguzi itakapo kaa tena kupanga tarehe mpya ya Uchaguzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MADAKTARI WA WANAMICHEZO WAZUIWA KUFANYA UCHAGUZI HADI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top