• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 26, 2018

  SIMBA SC WALIMWA ‘MAFAINI KIBAO’ KWA USHIRIKINA NA VURUGU ZA MASHABIKI WAKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba SC imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina katika mechi namba 171 dhidi ya wenyeji Njombe FC Aprili 3, 2018 kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
  Taarifa ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita kupitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao imesema vitendo hivyo ni pamoja na shabiki mmoja wa timu hiyo kuingia uwanjani na kuchukua taulo la kipa wa Njombe Mji lililokuwa golini. 
  Taarifa hiyo imesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
  Simba SC pia imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na mashabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho kwenye mechi namba 165 dhidi ya Mtibwa Sugar Aprili 9, 2018 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kitendo hicho cha washabiki wa Simba iliyokuwa ikicheza ugenini ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, wakati adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Aidha, Simba imepewa onyo kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika sita katika mechi namba 191 dhidi ya Mbeya City Aprili 12, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kitendo cha Simba ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo wakati adhabu dhidi yao imekijita katika Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Simba pia imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na kuwakilishwa na maofisa watatu badala ya wanne kwenye kikao cha maandalizi ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons Aprili 16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kitendo chao ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WALIMWA ‘MAFAINI KIBAO’ KWA USHIRIKINA NA VURUGU ZA MASHABIKI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top