• HABARI MPYA

    Tuesday, April 24, 2018

    NGORONGORO WAREJEA DAR KUJIPANGA KWA MECHI NA MALI, SERENGETI...

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imerejea nchini usiku wa kuamkia leo ikitokea nchini DR Congo kwenye mchezo wake wa marudiano wa kufuzu fainali za Africa za Vijana U20 dhidi ya DR Congo.
    Wachezaji wa Ngorongoro ambao wamefanikiwa kuivusha timu hiyo kwenda raundi ya pili wamepewa mapumziko ya siku tatu kwa mujibu wa program ya Kocha Mkuu Ammy Ninje.
    Katika raundi ya pili Ngorongoro Heroes watacheza dhidi ya Mali mwezi ujao mchezo wa kwanza wakianzia nyumbani.
    Nayo timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kesho inatupa karata yake muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya.
    Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
    Kufuzu hatua ya nusu fainali Serengeti Boys walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.
    Tunaitakia kila la kheri Serengeti Boys iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa nusu fainali.
    Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Serengeti Boys.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO WAREJEA DAR KUJIPANGA KWA MECHI NA MALI, SERENGETI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top