• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 22, 2018

  MSUVA AIFUNGIA LA USHINDI DIFAA HASSAN EL-JADIDA YAICHAPA RAJA CASABLANCA 2-1

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva leo ameifungia bao la ushindi timu yake, Difaa Hassan El- Jadida ikiilaza 2-1  Raja Casablanca Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro. 
  Msuva alifunga bao hilo dakika ya 76 baada ya Hamid Ahadad kuifungia Difaa Hassan El Jadida bao la kusawazisha dakika ya 45, kufuatia M Iyajour kutangulia kuwafungia Raja Casablanca dakika ya 41. 

  Kwa ushindi huo, Difaa Hassan El- Jadida inarejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Botola Pro kwa kufikisha pointi 41 kutokana na mechi 26. 
  Na Msuva akapumzishwa baada ya kazi hiyo nzuri, nafasi yake ikichukuliwa na Lahoucein Khoukhouch dakika ya 87.
  Japokuwa Msuva yupo katika msimu wake wa kwanza Difaa Hassan El- Jadida baada ya kununuliwa kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam Julai mwaka jana, lakini tayari ni mchezaji tegemeo wa timu hiyo iliyofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA AIFUNGIA LA USHINDI DIFAA HASSAN EL-JADIDA YAICHAPA RAJA CASABLANCA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top