• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 22, 2018

  NGORONGORO YAITUPA NJE DRC KWA MATUTA NA KUSONGA MBELE

  Na Mwandishi Wetu, KINSHASA
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imekata tiketi ya kwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania nafasi ya kucheza Fainali za vijana wa umri Afrika mwakani nchini Niger baada ya ushindi wa penalti 6-5, kufuatia sare ya 0-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jioni ya leo mjini Kinshasa.
  Mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Machi 31, Ngorongoro inayofundishwa na kocha Ammy Ninje anayesaidiwa na Juma Mgunda, Boniface Pawasa katika mazoezi ya nguvu, Meneja Leopold Mukebezi ‘Tassle’ na kicha wa makipa, Saleh Machuppa ilitoa sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Ramadhani Kabwili (kushoto) amekuwa shujaa leo baada ya kupangua penalti ya DRC


  Hizi ni habari njema kwa soka ya Tanzania, kwani sasa Ngorongoro inaelekea kuivusha nchi katika zama nyingine ya mafanikio.
  Ikumbukwe hao ndiyo vijana ambao mwaka jana walikuwa wanaunda timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka jana, Serengeti Boys ambao walifuzu kucheza Fainali za Afrika nchini Gabon mwezi Mei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO YAITUPA NJE DRC KWA MATUTA NA KUSONGA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top