• HABARI MPYA

    Friday, April 27, 2018

    MKUU WA MKOA, PAUL MAKONDA MGENI RASMI SIMBA NA YANGA JUMAPILI TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR DES SALAAM
    MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda atakua mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili 29,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
    Ndugu Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.
    Tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko (Jukwaa la rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu) 7,000.
    Tiketi zinapatikana kupitia Selcom.
    Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) atakuwa mgeni rasmi Jumapili Simba na Yanga Uwanja wa Taifa

    Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKUU WA MKOA, PAUL MAKONDA MGENI RASMI SIMBA NA YANGA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top