• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 29, 2018

  ABDI BANDA FUNGA MABAO MAWILI BAROKA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA CELTIC

  Na Mwandishi Wetu, JOHANNESBURG
  BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda jana amefunga mabao yote mawili, timu yake Baroka FC ikilazimishwa sare ya 2-2 na Bloemfontein Celtic katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini Uwanja wa Peter Mokaba mjini Johannesburg.
  Banda, beki wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, alifunga mabao yake dakika za 62 na 80 katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua baada ya Victor Letsoalo kutangulia kuwafungia wageni dakika ya 60.
  Lakini jitihada za sentahafu huyo wa zamani wa Coastal Union pia ziliishia kuipa pointi moja timu yake, baada ya Kabelo Dlamini kuisawazishia Bloemfontein Celtic dakika ya 90.
  Sare hiyo inaiongezea pointi moja Baroka FC na kufikisha 34 baada ya kucheza mechi 29 ikipanda kwa nafasi moja pia hadi ya 12 katika Ligi ya timu 16, wakati Bloemfontein Celtic inasogea nafasi ya tisa kutoka ya 11 kwa kufikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 29.
  Mamelodi Sundowns ndiyo wanaoongoza Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa pointi zao 59 za mechi 29, wakifuatiwa na Orlando Pirates pointi 52 za mechi 29, wakati Kaizer Chiefs ni ya tatu kwa pointi zake 45 za mechi 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ABDI BANDA FUNGA MABAO MAWILI BAROKA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA CELTIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top