• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 28, 2018

  INIESTA AMWAGA MACHOZI AKIAGA RASMI BARCELONA

  Iniesta wipes his nose as he thanks the club and discusses his future beyond Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  HISTORIA YA INIESTA NDANI YA BARCELONA

  Kujiunga: 1996
  Timu ya wakubwa: Oktoba 29, 2002 vs Club Bruges kwenye Ligi ya Mabingwa
  Mechi alizocheza: 669
  Mabao: 57
  Mataji: 
  La Liga
  (2004-05, 2005-06, 2008-09, 2009-10, 2010-11, 2012-13, 2014-15, 2015-16).
  Ligi ya Mabingwa
   (2005-6, 2008-09, 2010-11, 2014-15), Copa del Rey (2008-09, 2011-12, 2014-15, 2015-16, 2016-17, 2017-18), Club World Cup (2009, 2011, 2015), Super Cup ya Hispania
  (2005, 2006, 2009, 2010, 2011, 2013, 2016), 
  Super Cup ya UEFA
  (2009, 2011, 2015)
  KIUNGO wa kimataifa wa Hispania, Andres Iniesta alimwaga machozi wakati akitangaza kuhitimisha miaka yake 22 ya kuitumikia Barcelona. 
  Pia amethibitisha hatahamia klabu nyingine yoyote ya Ulaya.
  "Tulifika miaka 25 iliyopita kwenye gari yetu ya familia," alisema juu ya safari yake Barcelona akianzia timu ya vijana ya klabu hiyo katka akademi ya La Masia alipopelekwa na wazazi wake na bibi na babu yake kwa majaribio.
  "Sasa wapo hapa na mimi wakati ninaaga. Hiyo ilikuwa safari ya hisia, lakini ilikuwa mbaya kwa sababu nilibaki peke yangu na nilikuwa nina umri wa miaka 12 tu wakati huo! Lakini dhahiri ilikuwa ya thamani yake," alisema Iniesta.
  Alikuwa akibubujikwa machozi wakati akiwashukuru wachezaji wenzake waliokuwemo kwenye chumba cha mkutano na Waandishi wa Habari. 
  Ni Lionel Messi na Luis Suarez katika wachezaji wa kikosi cha kwanza waliokosekana kwenye. Na ni wakati akiwataja wachezaji wenzake ndipo macho yalipoanza kumtoka machoni mwake.
  Hakukuwa na uthibitisho wa safari yake kwenda China mwishoni mwa msimu lakini alithibitisha hatakwenda kucheza Ligi Kuu ya England ambako anatakiwa na Manchester City inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: INIESTA AMWAGA MACHOZI AKIAGA RASMI BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top