• HABARI MPYA

  Thursday, April 19, 2018

  TFF YAIPONGEZA YANGA KUINGIA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameipongeza klabu ya Yanga SC kwa kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
  Yanga SC imefanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza kwa mabao 2-0 kabla ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia jana.
  Karia kwa niaba ya TFF ameipongeza klabu ya Yanga kwa hatua hiyo kubwa iliyofikia ambayo inaakisi mpira wa Tanzania kiujumla.
  “Mafanikio ya klabu ya Yanga ni mafanikio ya Tanzania kiujumla na TFF ambao ni wasimamizi wa Mpira nchini tunajivunia mafanikio hayo ya Yanga, ambao tumekuwa tunashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Tanzania”amesema Karia.
  Amesema anaamini watafanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye hatua hiyo ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAIPONGEZA YANGA KUINGIA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top