• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 27, 2018

  NJOMBE MJI NA NDANDA KATIKA VITA YA KUKATAA KUIACHA LIGI KUU LEO SABA SABA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea leo kwa mechi mbili zote zikichezwa Nyanda za Juu kusini mwa nchi.
  Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, wenyeji Njombe Mji FC watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara, wakati Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wenyeji, Mbeya City watawakaribisha Singida United.
  Ligi Kuu itaendelea kesho, Azam FC wakiwa wageni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro, Majimaji FC wakiwakaribisha Ruvu Shooting FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songe na Stand United FC wakiwa wenyeji wa Kagera Sugar FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Njombe Mji inapigana kuepuka kushuka Daraja, sasa ikiwa inashika mkia kwa pointi zake19 baada ya kucheza mechi 25

  Njombe Mji inapigana kuepuka kushuka Daraja, sasa ikiwa inashika mkia kwa pointi zake19 baada ya kucheza mechi 25, wakati Maji Maji na Ndanda nazo zina hali mbaya pia.
  Maji Maji iko juu ya Njombe FC kwa pointi moja tu zaidi, 20 baada ya kucheza mechi 25, wakati Ndanda FC ina pointi 23 za mechi 25 pia, ikiwa nyuma ya Mbao FC yenye pointi 24 za mechi 25.  
  Mbeya City inashika nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu ya 16, ikiwa na pointi 27 za mechi 25, wakati Stand United ni ya tisa kwa pointi zake 28 za mechi 25.
  Timu mbili zitashuka mwishoni mwa msimu mwezi ujao na tayari timu nne zimekwishapanda ambazo ni JKT Tanzania, Coastal Union, African Lyon, Alliance Schools, Biashara United ya Mara na KMC ili kuwa na timu 20 msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NJOMBE MJI NA NDANDA KATIKA VITA YA KUKATAA KUIACHA LIGI KUU LEO SABA SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top