• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 20, 2018

  DILUNGA AIPELEKA MTIBWA SUGAR FAINALI KOMBE LA TFF, APIGA ZOTE MBILI STAND UNITED YAFA 2-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Stand United jioni ya leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Shujaa wa Mtibwa Sugar leo ni kiungo wa zamani wa Yanga SC, Hassan Dilunga aliyefunga mabao yote dakika za 30 na 39 na sasa Wakata Miwa hao wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro wanaweka rekodi ya kuchea fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.  Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Zuberi Katwila sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili Jumatatu Uwanja wa Namfua mjini Singida, baina ya JKT Tanzania ya Dar es Salaam na wenyeji Singida United.
  Fainali ya michuano hiyo itafanyika Juni 2, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na bingwa pamoja na kupata Sh. Milioni 50, pia ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Mshindi wa pili atapata Milioni 10, wakati Mchezaji Bora atazawadiwa Sh. Milioni 1 sawa na Kipa Bora, Mfungaji Bora, huku Mchezaji Bora wa Fainali akiondoka na Sh. 500,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DILUNGA AIPELEKA MTIBWA SUGAR FAINALI KOMBE LA TFF, APIGA ZOTE MBILI STAND UNITED YAFA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top