• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 25, 2018

  SERENGETI BOYS YATINGA FAINALI CECAFA U17 BURUNDI, YAIPIGA KENYA 2-1 MUYINGA

  TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA U17 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Kenya leo Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
  Haukuwa ushindi mwepesi kwa Serengeti Boys inayonolewa na Oscar Milambo chini ya Mshauri wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen, kwani ililazimika kutoka nyuma kwa 1-0 ili kuwalaza Wakenya 2-1 baada ya dakika 90.
  Mabao ya Serengeti Boys leo yamefungwa na Jaffar Juma dakika ya 21 na Kelvin Paul dakika ya 62 na sasa vijana wa Tanzania watakutana na mshindi wa Nusu Fainali nyingine baina ya Uganda na Somalia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YATINGA FAINALI CECAFA U17 BURUNDI, YAIPIGA KENYA 2-1 MUYINGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top