• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 23, 2018

  MOHAMED SALAH NDIYE MCHEZAJI BORA WA PFA ENGLAND

  Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA usiku wa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  WASHINDI WOTE WA PFA USIKU WA JANA 

  Mchezaji Bora wa Mwaka: Mohamed Salah
  Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka: Leroy Sane
  Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka: Fran Kirby
  Mchezaji Bora Chipukizi wa Kike wa Mwaka: Lareun Hemp
  Tuzo maalum ya PFA: Cyrille Regis 
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA).
  Mchezaji huyo wa Liverpool ameshinda tuzo hiyo akimuangusha mshambuliaji wa Manchester City, Kevin De Bruyne baada ya kufunga mabao 41 katika msimu wake wa kwanza Anfield. 
  Leroy Sane aliyekuwa na msimu wa kipekee ndani ya Manchester City, amejinyakulia tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Grosvenor House mjini London. 
  Salah anakuwa mchezaji wa saba wa Liverpool kushinda tuzo hiyo na wa kwanza tangu ashinde Luis Suarez mwaka 2014.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anapewa nafasi kubwa ya kushinda Kiatu cha Dhahabu na pia anaweza kuongeza tuzo ya Mchezaji Bora wa Chama cha Waandishi wa Habari katika kabati lake, lakini kipaumbele chake ni mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya klabu yake ya zamani, Roma kesho. 
  "Ni heshima kubwa. Nimejituma na nina furaha kushinda hii," amesema Salah, ambaye amekuwa Mmisri wa kwanza kushinda tuzo hiyo. "Natumaini sitakuwa wa mwisho! Ninajivunia sana kushindana nimejituma sana,".
  Baada ya kufunga katika sare ya 2-2 Jumamosi na West Brom, Salah amefikia rekodi ya Suarez wakilingana na Alan Shearer na Cristiano Ronaldo kufunga mabao 31 katika mechi 38 za Ligi Kuu ya England ndani ya msimu mmoja. 
  Na Mmisri huyo anataka aweke rekodi mpya ndani ya Liverpool katika mechi tatu zilizobaki.
  "Kuvunja rekodi za Ligi Kuu England ni kitu fulani kikubwa England na duniani kote. Nataka kuvunja rekodi hii na kuvunja na nyingine (mechi 42 kwa msimu). Acha tuone nini kitatokea,"amesema Salah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOHAMED SALAH NDIYE MCHEZAJI BORA WA PFA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top