• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 30, 2018

  MWADUI FC NA MBAO KATIKA SHUGHULI PEVU MTANANGE WA LIGI KUU LEO

  Na Mwandishi Wetu, MWADUI
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itaendelea leo kwa mchezo mmoja tu, Mwadui FC wakiikaribisha Mbao FC Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
  Hiyo ni baada ya jana kushuhudiwa, Simba SC wakizidi kulikaribia taji la ubingwa wa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam bao pekee la Erasto Edward Nyoni.
  Mbao FC ikishinda mechi yake ya 26 leo itapanda kwa nafasi moja hadi 12 kutoka ya 13, kwani itafikisha pointi 29 na kuishusha Mwadui FC.
  Mwadui FC yenyewe itafikisha pointi 29 na kupanda hadi nafasi ya tisa kutoka ya 12 na kuzishusha Kagera Sugar yenye pointi 27, Mbeya City pointi 28 na Stand United pointi 29. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWADUI FC NA MBAO KATIKA SHUGHULI PEVU MTANANGE WA LIGI KUU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top