• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 23, 2018

  AHMAD AMPONGEZA SALAH KWA KUTAWA TUZO YA PFA

  RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad amempongeza Mmisri, Mohamed Salah kwa kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) msimu wa 2017/2018.
  Salah alipewa tuzo hiyo usiku wa jana mjini London akiweka rekodi ya kuwa mzaliwa wa kwanza wa Afrika kushinda tuzo hiyo.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa na msimu mzuri akiwa na vigogo hao wa England, Liverpool, tangu ajiunge nao Juni mwaka 2017. 
  Akiwa mchezaji tegemeo wa Liverpool, Salah amefunga mabao 41 kwenye mashindano yote hadi sasa, na pia ni amekuwa Mwafrika wa kwanza kufunga zaidi ya mabao 30 kwa msimu kwenye Ligi Kuu ya England.
  Mohamed Salah ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England

  “Salah ameifanya Afrika ijivunie. Akiwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika kwa sasa, amedhihirisha kwamba wachezaji wa Afrika wana uwezo wa kushinda tuzo kubwa duniani. Familia ya soka Afrika inajivunia mafanikio ya Salah kama mtoto halisi ya bara hili,".
  “Uwajibikaji wake kote katika klabu na nchi yake unamfanya awe mfano wa kuigwa kwa wanasoka chipukizi kote barani na kwingine. Tunamtakia mazuri katika mustakabali wake siku zijazo,” amesema Ahmad.
  Zikiwa zimebaki mechi nne msimu kumalizika, nyota huyo wa Misri pia anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya England akiwa amefunga mabao 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AHMAD AMPONGEZA SALAH KWA KUTAWA TUZO YA PFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top