| Solomon Asante akishangilia baada ya kuifungia bao pekee TP Mazembe jana |
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mazembe, bao pekee la TPM lilifungwa na Roger Assale dakika ya 53 na sasa mabingwa hao mara nne Afrika wanatimiza pointi nane baada ya kushinda mechi mbili na sare mbili.
Washambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta alicheza mechi yote, wakati Thomas Emmanuel Ulimwengu alitokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Solomon Asante.
Al Hilal ya Sudan inabaki na pointi zake tano baada ya juzi kufungwa 1-0 nyumbani na Moghreb Tetouan ya Morocco ambayo sasa nayo imefikisha pointi tano. Smouha ya Misri ina pointi tatu.
Mechi ya Kundi B iliyochezwa Ijumaa, USM Alger iliifunga 1-0 MC Eulma, zote za Algeria.
Hiyo ni mechi ya nne mfululizo UM Alger inashinda na sasa inafikisha pointi 12 kileleni, ikifuatiwa kwa mbali na El Merreikh ya Sudan yenye pointi nne.


.png)
0 comments:
Post a Comment