Na Princess Asia, MOROGORO
KAGERA Sugar imeipunguza kasi Mtibwa Sugar baada ya kutoa nayo sare ya 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyodumu kwa siku mbili, Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Dakika 45 za kwanza jana zilimalizika Mtibwa Sugar ikiwa inaongoza bao 1-0 lililofungwa na
Ame Ali dakika ya 43, lakini mchezo huo ukalazimika kuahirishwa kutokana na mvua kubwa.
Hali ya Uwanja haikuweza kuruhusu tena mchezo kuendelea na timu zote mbili zikakubaliana kumalizia dakika 45 nyingine leo asubuhi na Kagera wakafanikiwa kupata sare.
Alikuwa ni mshambuliaji Rashid Mandawa aliyeifungia Kagera bao la kupata pointi moja ugenini dakika ya 57 leo na kuwapunguza kasi Mtibwa kileleni mwa Ligi Kuu.
Mtibwa wanafikisha pointi 15 baada ya mechi saba, wakiendelea kubaki kileleni, kwa pointi mbili zaidi dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC na Yanga SC.
Ligi hiyo inaendelea jioni ya leo kwa mechi mbili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Simba SC watamenyana na Ruvu Shooting na Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam pia, JKT Ruvu wanaikaribisha Ndanda FC ya Mtwara.

![]() |
Kagera Sugar wameipunguza kasi Mtibwa Sugar Ligi Kuu |

0 comments:
Post a Comment