KIKOSI cha watu 35 cha timu ya ES Setif ya Algeria
kinatarajiwa kuwasili nchini leo saa 12
alfajiri kwa ndege ya EgyptAir kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi
ya Simba itakayochezwa Machi 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface
Wambura alisema jana kwamba msafara huo unahusisha wachezaji, benchi la ufundi, viongozi wa
timu, kiongozi wa msafara kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Algeria (FAF)
wakati watatu ni waandishi wa habari.
Aliwataja wachezaji 20 katika msafara huo ni Mohamed
Benhamou, Sofiane Bengorine, Riadh Benchadi, Smain Diss, Farouk Belkaid, Khaled
Gourmi, Mourad Delhoum, Said Arroussi, Mokhtar Benmoussa, Tarek Berguiga,
Mohamed Aoudi na Amir Karaoui.
Wengine ni Mohamed El Amine Tiouli, Racid Ferrahi, Youcef
Ghezzali, Youssef Sofiane, Mokhtar Megueni, Rachid Nadji, Abderrahmane Hachoud
na Akram Djahnit. Kocha wa timu hiyo ni Alain Norbert Geiger ambaye ni raia wa
Uswisi.
Mchezo huu utakaoanza kurindima saa 10 kamili jioni
ukichezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda
Hudu Munyemana atakayesimama kati akisaidiwa na Felicien Kabanda,
Theogene Ndagijimana na Edouard Bahizi, huku kamishna wa mechi hiyo
atakuwa Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe.
Timu hizo zitarejeana Algeria Aprili 6 na iwapo Simba itashinda
itacheza mechi ya kwanza nyumbani Aprili 29 mwaka huu na
mshindi kati ya El Ahly Shandy ya Sudan na Ferroviario de Maputo ya Msumbiji
ambapoya marudiano itachezwa kati ya Mei 11, 12 na 13 mwaka huu.



.png)
0 comments:
Post a Comment