• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  MAN CITY CHUPUCHUPU, ARSENAL YALALIWA, CHELSEA YAUA

  Torres
  Theo

  Mwokozi wa Manchester City, Aleksandar Kolarov

  KLABU ya Manchester City leo imepata mabao mawili ndani ya dakika sita za mwisho na kubahatisha sare ya 3-3 na Sunderland na kutunza rekodi yao ya kutofungwa nyumbani katika miezi 15 kwenye Ligi Kuu ya England.
  City ilitaka kuwatia presha vinara wa ligi hiyo, Manchester United lakini Sebastian Larsson akawafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 31.
  Mario Balotelli alisawazisha kwa penalti dakika ya 43, lakini Nicklas Bendtner akaifungia la pili Sunderland dakika mbili baadaye na Larsson akafanya 3-1 dakika ya 55.
  Balotelli akafunga tena dakika ya 85 na Aleksandar Kolarov akasawazisha dakika moja baadaye.
  City haijafungwa kwenye Uwanja wa Etihad tangu  Desemba 2010 ilipopigwa 2-1 na Everton, lakini.
  Katika mchezo mwingine, rekodi ya Arsenal kushinda mechi saba mfululizo katika Ligi Kuu imevunjwa leo na QPR kwa kichapo cha 2-1 Uwanja wa Loftus Road.
  Rangers iliyokuwa imeshinda mechi mbili tu katika mechi 18, mabao yake leo yalifungwa na Adel Taarabt na Samba Diakite, wakati la Arsenal lilifungwa na Theo Walcott.
  Chelsea nayo imeshinda 4-2 dhidi ya Aston Villa.
  Villa ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 zikiwa zimebaki dakika 10, lakini Branislav Ivanovic akafunga bao lake la pili kwenye mchezo huo na Fernando Torres akafunga lingine dakika za lala salama kuipa matumaini Chelsea inayoshika nafasi ya tano ya kumaliza ligi ndani ya Top Four.
  Daniel Sturridge aliifungia Chelsea bao la kuongoza  na Ivanovic akapiga la pili dakika ya 51 kabla ya James Collins na Eric Lichaj kuifungia Villa.
  Nahodha wa Villa, Stiliyan Petrov aliushuhudia mchezo huo akiwa jukwaani siku moja baada ya kutangazwa anaumwa acute leukemia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY CHUPUCHUPU, ARSENAL YALALIWA, CHELSEA YAUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top