• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  BARCELONA WAUCHONGEA UEFA UWANJA WA AC MILAN


  Refa Msweden, Jonas Eriksson (katikati) ya wachezaji wa Barcelona, viungo Muargentina Javier Mascherano (kushoto) na Xavi Hernandez katika mechi ya Ligi ya Mabingwa, Robo Fainali ya kwanza jana dhidi ya AC Milan Uwanja wa San Siro mjini Milan. Mechi hiyo iliisha kwa sare 0-0 na Eriksson alilaumiwa na vyombo vya habari vya Hispania baada ya mchezo huo.

  KLABU bingwa Ulaya na Duniani, Barcelona leo imetuma malalamiko yake Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) juu ya pitch mbovu ya Uwanja wa San Siro, baada ya sare ya bila kufungana katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji AC Milan.
  "FC Barcelona wametuma malalamiko Uefa kuhusu pitch ya Uwanja wa Giuseppe Meazza (San Siro) katika mechi ya Ligi ya Mabingwa," ilisema klabu hiyo ya Catalan katika tovuti yake.
  Baada ya mechi hiyo ya jana, kocha wa Barcelona, Pep Guardiola alilalaimikia pitch, akisema "Tumeweza kila kitu, tumekuja na tumecheza. Lakini tatizo ni ubora wa eneo la kuchezea. Ni vigumu wakati pitch ni ngumu namna hii ". Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0-0, wakati zitarudiana Jumanne ijayo.
  Guardiola

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA WAUCHONGEA UEFA UWANJA WA AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top