• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  TIBAIGANA AWAKABIDHI RASMI MABONDIA YANGA HATI YA KUWAVAA COASTAL KESHO


  Kikosi cha Yanga

  MWENYEKITI wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Tibaigana amesema kwamba kikao cha jana hakikumalizika na kwa maana hiyo hawajachukua hatua mpya kuhusu wachezaji watano wa Yanga, wanaokabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.Akizungumza na bongostaz dakika chache tu zilizopita, Tibaigana ambaye ni Kamanda Mstaafu wa Kanda Maalum Dar es Salaam Jeshi la Polisi nchini, alisema kikao cha jana hakikumalizika na watakutana tena Jumanne kumalizia.Kwa mantiki hiyo, wachezaji wa Yanga MABEKI STEFANO MWASIKA ALIYEMPIGA NGUMI REFA ISRAEL NKONGO ALIFUNGIWA MWAKA MMOJA NA FAINI YA SH MILIONI 1, NADIR HAROUB ‘CANNAVARO’ ALIFUNGIWA MECHI SITA NA FAINI YA SH. 500,000, VIUNGO NURDIN BAKARI ALIFUNGIWA MECHI TATU NA FAINI SH. 500,000 SAWA NA OMEGA SEME NA MSHAMBULIAJI JERRY TEGETE wataichezea timu yao katika Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union kesho, Uwanja wa  Mkwakwani, Tanga.                       KAMATI YA TIBAIGANA ILIWAACHIA HURU WACHEZJI WATANO WA YANGA WALIOKUWA WAMEFUNGIWA KWA VIPINDI TOFAUTI NA KAMATI YA LIGI YA TFF, BAADA YA KURIDHIKA NA UTETEZI WA KLABU HIYO JUU YA ADHABU HIZO.AKITANGAZA KUSITISHA ADHABU HIYO, TIBAIGANA ALISEMA KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA TFF, KAMATI YA LIGI HAINA MAMLAKA YA KUMFUNGIA MCHEZAJI YEYOTE WALA KUTOA ADHABU, ISIPOKUWA KAMATI YA NIDHAMU.KAMATI YA LIGI ILIYOKUTANA MACHI 12, MWAKA HUU CHINI YA MWENYEKITI WAKE, GEOFFREY NYANGE ‘KABURU’ ILIWAFUNGIA WACHEZAJI HAO WA YANGA KWA TUHUMA ZA UTOVU WA NIDHAMU WALIOUFANYA KWENYE MECHI YA AZAM FC, MACHI 10, MWAKA HUU, UWANJA WA TAIFA.Mapema  jana AKIIZUNGUMZIA MECHI NA COASTAL UNION, Ofisa Habari wa Yanga, Louis SENDEU ALISEMA MORALI NI KUBWA NA WANAAMINI WANAKWENDA KUCHUKUA POINTI TATU HUKO.ALISEMA WAMEKWISHAANDALIWA MAZINGIRA YA SEHEMU SALAMA YA KUFIKIA, KUFANYA MAZOEZI NA HATA KULA, ILI KUHEPA FITINA ZA WAGOSI AMBAO WAMEPANIA KWELI KUIADHIRI YANGA, KULIPA KISASI CHA 5-1 WALIZOFUNGWA KATIKA MCHEZO WA KWANZA WA LIGI KUU YA BARA, UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM.Mapema jana KAMATI YA MASHINDANO YA YANGA, LEO IliWAPA WACHEZAJI WA KLABU HIYO SH. MILIONI 5 WAGAWANE NA KUWAAHIDI SH. MILIONI 5 NYINGINE WAKISHINDA MECHI DHIDI YA COASTAL UNION YA TANGA JUMAMOSI UWANJA WA MKWAKWANI, TANGA.MCHEZO HUO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZAANIA BARA UNATARAJIWA KUWA MKALI NA WA KUSISIMUA, KWANI COASTAL INAYOFUNDISHWA NA WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA WA ZAMANI NCHINI, BEKI JAMHURI MUSSA KIHWELO NA JUMA RAMADHAN MGUNDA IMEPANIA KUSHINDA KUITIBULIA YANGA HARAKATI ZA UBINGWA.KUHUSU HALI YA WACHEZAJI, ALISEMA NI SALUM ABDUL TELELA PEKEE AMBAYE HATAJUMUISHWA KWENYE MCHEZO HUO KWA SABABU AMEPEWA MAPUMZIKO BAADA YA KUPONA.“HUO NDIO UTARATIBU WETU KWA SASA, MCHEZAJI AKIPONA ANAPEWA MUDA ZAIDI WA KUPUMZIKA AWE SAWASAWA, HATA YAE BERKO AMEKAA NJE MUDA MREFU KWA SABABU ALIPEWA NA SIKU ZA KUPUMZIKA,” 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIBAIGANA AWAKABIDHI RASMI MABONDIA YANGA HATI YA KUWAVAA COASTAL KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top