• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  KALOU ASEMA HAONI KWA NINI CHELSEA ISIWE BINGWA ULAYA


  Kalou kulia na Torres aliyempa pasi ya bao kushoto

  NYOTA wa Chelsea, Salomon Kalou amesema kwamba inaweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
  Mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich amekuwa ana njaa ya taji hilo kubwa Ulaya tangu aichukue klabu hiyo mwaka 2003.
  Bao la dakika za lala salama la Kalou dhidi ya Benfica jana, lililoifanya Chelsea inuse Nusu Fainali ya Ulaya, limemfanya mchezaji huyo aamini wanaweza kutwaa Kombe.  
  “Naamini hakuna sababu ya kutufanya tushindwe kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa,” alisema Kalou.
  "Chochote kinawezekana. Tuna timu ya kufanya hivyo, tuna wachezaji wa kufanya hivyo."
  Kalou hakufurahia kazi yake enzi za Andre Villas-Boas, kwani alicheza mechi 14 tu kwenye mashindano yote.
  Lakini tangu Robert Di Matteo aanze kazi, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amerejesha furaha yake kwa kuwa mchezaji wa kudumu wa kikosi cha kwanza na anaisaidia timu yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KALOU ASEMA HAONI KWA NINI CHELSEA ISIWE BINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top