• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  MAFISANGO ASIMAMISHWA MUDA USIOJULIKANA , KABURU AMWAGA FEDHA KAMBINI SIMBA


  Mafisango aliyebebwa juu na wachezaji wenzake baada ya kufungta bao, je kukosekana kwake hakutaiathiri timu?

  UONGOZI wa Simba umemsimamisha kwa muda usiojulikana kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango kwa utovu wa nidhamu, imeelezwa.Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba, Mafisango amechukuliwa hatua hiyo kwa utovu wa nidhamu, ambao umekuwa ukijirudia mara kwa mara.Wakati huo huo, mgomo wa wachezaji wa Simba kuhusu mgawo wao baada ya mechi dhidi ya ES Setif ya Algeria umeisha baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kwenda kuwaongezea fedha wachezaji wa timu hiyo.Simba ipo kambini Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya African Lyon Jumamosi mjini Dar es Salaam.Baada ya mechi hiyo, Simba itaelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Se Setif, wakipitia Misri.      

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAFISANGO ASIMAMISHWA MUDA USIOJULIKANA , KABURU AMWAGA FEDHA KAMBINI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top