• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 26, 2012

  SCHWEINSTEIGERS MWINGINE ATUA BAYERN

  Tobias Schweinsteigers
  KLABU ya Bayern Munich inaweza kuwa na Schweinsteigers msimu ujao baada ya kaka wa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Bastian, kusaini mkataba wa kujiunga na kikosi cha wachezaji wa akiba wa The Bavarians, klabu hiyo imesema leo. Mshambuliaji Tobias Schweinsteiger, mwenye umri wa miaka 30, anatarajiwa kuhama kutoka klabu ya Daraja la Tatu, Jahn Regensburg, ambako alikuwa Nahodha na mfungaji bora wa timu kwa mabao yake 12 msimu huu.
  Bastian Schweinsteiger kwa sasa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na yuko nje kwa matibabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SCHWEINSTEIGERS MWINGINE ATUA BAYERN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top