• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  TIMU LA SAMATTA UWANJANI KESHO


  TP Mazembe

  BAADA ya kuahirishwa kwa mechi ya Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), dhidi ya DC Motema Pembe, TP Mazembe itacheza mechi ya kirafiki kesho saa 9.30 alasiri dhidi ya Tshinkunku.
  Kwa Tshinkunku mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Royal Leopards ya Swaziland, Kombe la Shirikisho Aprili 7, mwaka huu.
  Mazembe inajiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos ya Zimbabwe.
  Kikosi cha Mazembe kina Watanzania wawili, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu ambao wote ni washambuliaji.
  Samatta ndiye aliyefunga bao katika mechi na Dynamos timu hizo zikitoka sare ya 1-1 wiki iliyopita, ingawa siku hiyo aliuamia bega na atakuwa nje kwa wiki mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIMU LA SAMATTA UWANJANI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top