• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  REAL MADRID WAFUNGUA AKADEMI


  VIGOGO wa Ulaya, Real Madrid wako mbioni kufungua akademi ya soka nchini China mwakani, wakiungana na klabu ya Ligi Kuu ya China, Guangzhou Evergrande, amesema mmiliki wa klabu hiyo ya China katika tovuti yake.
  Madrid, ambao ni mabingwa mara nyingi zaidi Ulaya, mara tisa, wako katika mpango wa kujitangaza zaidi na wameingia China, ambayo inavutia klabu nyingine kubwa Ulaya.
  Akademi hiyo itakayokuwa kusini mwa jiji la Guangzhou, itakuwa na wachezaji wapatao 3 000 katika mwaka wa kwanza, watakaokuwa wakitumia vifaa na kufundishwa kwa ubora ule ule wa akademi ya Real Madrid nchini Hispania.
  Kocha wa vijana wa klabu hiyo ya Hispania, Fernando Sanchez Cipitria ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi.
  "Tutapeleka timu ya makocha wenye wasifu mkubwa na kutengeneza mfumo mzuri wa kazi kwa kiwango kile kile cha Hispania," gazeti la China Daily lilimnukuu Cipitria.
  "Pia tutawafundisha makocha wa China katika shule na kuchagua wachezaji Fulani waliofikia kustaafu na makocha kuwaendeleza zaidi Real Madrid.".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID WAFUNGUA AKADEMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top