• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 26, 2012

  MIJI YA FAINALI ZA AFRIKA MWAKANI KUJULIKANA MAPEMA MWEZI UJAO

  Zambia, mabingwa wa Afrika 2012
  MIJI itakayotumika kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini, inatarajiwa kujulikana Aprili 4, mwaka huu.
  Wale wanaotafuta nafasi katika miji saba, watawasilisha maombi yao kwa kamati ya maandalizi siku ya Jumatatu.
  Walitarajiwa kufanya hivyo siku ya Ijumaa lakini waliomba muda zaidi wa kujiandaa.
  Meneja wa mawasiliano wa Chama cha Kandanda cha Afrika Kusini Dominic Chimhavi, ameongeza kusema maombi yatakayofanikiwa yatatangazwa tarehe 4 mwezi wa Aprili.
  Shirikisho la Kandanda la Afrika (Caf) linajipanga kutembelea viwanja nchini Afrika Kusini mwezi wa Aprili.
  Uzinduzi rasmi wa michuano hiyo pia umepangwa kuwa tarehe hiyo 4 mwezi wa Aprili.
  Tangazo la miji itakayofanikiwa kuandaa mashindano hayo litatolewa mbele ya wajumbe wa Shirikisho la Kandanda la Afrika wakati wa uzinduzi.
  Afrika Kusini imepata nafasi hiyo kwa kuwa na viwanja vizuri sana na hasa walipoandaa mashindano ya Kombe la Dunia kwa mafanikio makubwa mwaka 2010.
  Walipatiwa nafasi hiyo ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 baada ya Libya kuonekana isingeweza kutokana na ghasia zilizotokea nchini humo.
  Miji tisa imearifiwa imejipanga kuandaa mashindano hayo ya mwakani yenye mvuto barani Afrika.
  Miji inayopewa nafasi kubwa ni Johannesburg, Cape Town, Durban, Port Elizabeth, Polokwane, Nelspruit na Bloemfontein.
  Viwanja katika miji hiyo vilitumika kwa michuano ya Kombe la Dunia na vitakuwa katika hali nzuri kuandaa mashindano ya kandanda ya bara la Afrika.
  Fainali hizo za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoshirikisha nchi 16 zitaanza patashika zake kuanzia katikati ya mwezi wa Januari hadi katikati ya mwezi wa Februari mwaka 2013
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MIJI YA FAINALI ZA AFRIKA MWAKANI KUJULIKANA MAPEMA MWEZI UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top