• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  AC MILAN WAIDHIBITI BARCA, BAYERN YANUSA NUSU FAINALI


  Messi akidhibitiwa na Nesta
  Messi katika mishemishe
  Ibra akiwapigia makofi mashabiki baada ya mechi
  Ibra katika mishe

  AC Milan wamewaweka katika wakati mgumu Barcelona baada ya kuwalazimisha sare ya bila kufungana usiku huu kwenye Uwanja wa San Siro katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Barca watakuwa katika mgumu kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Camp Nou, kwa sababu hawakufanikiwa kupata bao ugenini.
  Wakati Barca wakitoka uwanjani vichwa chini Milan, Bayern Munich ilinusa Nusu Fainali kwa ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Marseille, mabao ya Mario Gomez na Arjen Robben.
  Barcelona ilitawala mchezo kwa asilimia 62, lakini ilishindwa kupata bao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili na nusu.
  Kila timu hiyo ya Hispania ilipokuwa ikitengeneza mipango, ilikuwa ikitibuliwa na safu ya walinzi wazoefu ya Milan iliyokuwa ikiundwa na watu kama kipa Christian Abiatti na Jonas Eriksson.
  Nafasi pekee ya Lionel Messi kufunga ilikuwa kipindi cha kwanza na pamoja na kutupia mpira nyavuni, lakini bao lilikataliwa kwa sababu aliotea dhahiri kabisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AC MILAN WAIDHIBITI BARCA, BAYERN YANUSA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top