• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  KIBERA ACHA CHUKI YA KASONGO MPINDA NA MK GROUP


  Kasongo Mpinda

  WIMBO:-KIBERA ACHA CHUKI
  MTUNZI:-KASONGO MPINDA.”CRYTON”
  WAIMBAJI:-KASONGO MPINDA.
  BENDI:-MK GROUP.”NGULUPA TUPATUPA DANCE”
  KATIKA wimbo huu mbali na ujumbe unaotuasa jamii kuondokana na roha za fihi na chuki huku ukituelekeza kuondokana na ubinafsi bali maisha yetu yanastahili kutawaliwa na upendo; utamkubali mwana mama;Asia Daruweshi kwa jinsi alivyomudu kucheza na kinanda kwa umahili mkubwa.
  Ama utaridhika na sauti yenye msisitizo katika ghani ya mtunzi wa kibao hiki; Nguli Kasongo Mpinda”Cryton”kwa jinsi alivyoichezea kwa kupanda na kushuka huku akiwasilisha Ujumbe endelevu tofauti na vibao vya watunzi wa leo hii hususani wa kizazi kipya ambapo nyimbo zao nyingi hazina maudhui, na pindi upatikanapo basi huwa hasi.
  Mtunzi na Mwimbaji anamkanya muhusika kuondokana na tabia aliyonayo ambayo haina maslahi hapa duniani. Kwani yastahili UCHEKE NA WATU UPATE VIATU. Kinyume na hapo, tabia aliyonayo ya ubinafsi,chuki na roho mbaya atendayo itamletea madhara hapa duniani naaam PELE NDILO LIWALO DONDA!
  Tunakumbushwa kwamba sisi sote ni bin Adamu,yatupasa tupendane asilani tusiwekeane kinyongo.yastahili tusaidizane kwa kila jambo,pindi unapomuona mwenzio yumo kwenye kisima kirefu mpe mkono umvute na si kumnyanyapaa kwa ugumu wa maisha yanayomkabili.
  Tungo hii iliyorekodiwa mnamo mwaka 1986,imefanyiwa kazi inavyostahili na kuleta mvuto kwa msikilizaji,mbali na mtunzi pamoja na “Super Mama;”Asia Daruweshi ni Andy Swebe aliyeungurumisha gitaa zito, Mafumu Bilali “Super Sax”ama Bombenga aliyepuliza Saxaphone, Joseph Mulenga “King Spoiler” aliyepiga gitaa linaloongoza na Monga Stanley”Monga Stan”aliyecheza na gitaa la kati “Rythym;
  Trampet zilipulizwa na Abdallha Tuba na Kayembe Ndalambo,huku Abdallha Rock akikaanga chipsi”Drums”na Tumba  zikiwa katika  himaya za Sidy Moris”Super Conga”

  SASA IMBA:-
  Mpende mwenzioo
  Kama unavyojipenda wewee eeeh!
  Mwenye upendoo
  Hana Hasiraa
  Mwenye upendoo ni mtulivuu
  Mwenye upendoo huwatumikia wenzakee
  Upendo ni utumishi
  Utumishi ni upendo
  Upendo ni uhai
  Chuki ni mauti
  Upendo wa kwelii
  Sio wa maneno matupu maamaaaa
  Mbali na matendo maamaaaa
  Mbali na matendooooo oooh!
  {Wee Kiberaa Acha chuki wee..utaleta ugomvi eee}
  Mpende mwenzioo
  Kama unavyojipenda wewee eeeh!
  Mwenye upendoo
  Hana Hasiraa
  Mwenye upendoo ni mtulivuu
  Mwenye upendoo huwatumikia wenzakee
  Upendo ni utumishi
  Utumishi ni upendo
  Upendo ni uhai
  Chuki ni mauti
  Upendo wa kwelii
  Sio wa maneno matupu maamaaaa
  Mbali na matendo maamaaaa
  Mbali na matendooooo oooh!

  CHORUS:-
  Kibera acha chuki eee
  Chuki yaleta uchawii yeeh..
  Kibera acha chuki eee
  Chuki yaleta migonganoo oooh..
  Kibera acha chuki eeeeh…
  Chuki yavunja umoja yeeeh..yooo…Kiberaaa!
  Kibera weee bwana Kiberaaa
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Kibera acha chuki eee
  Chuki yaleta ugomvii yeeh..
  Kibera acha chuki eee
  Chuki yaleta migonganoo oooh..
  Kibera acha chuki eeeeh…
  Chuki yavunja umoja yeeeh..yooo…Kiberaaa!
  Kibera weee bwana Kiberaaa
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Oooo…yooo Kiberaaaa
  Kibera wee bwana Kiberaa…
  Oooo…yeeeh Kiberaa
  Kibera wacha wee Kiberaaaah!

  Kibera acha chuki eee
  Chuki yaleta uchawii yeeh..
  Kibera acha chuki eee
  Chuki yaleta migonganoo oooh..
  Kibera acha chuki eeeeh…
  Chuki yavunja umoja yeeeh..yooo…Kiberaaa!
  Kibera weee bwana Kiberaaa
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Oooo…yoooh Kiberaa
  Kiberaa wee bwana Kiberaaa
  Ooo… yeeeh Kiberaaa
  Kiberaa wacha wee Kiberaaa
  Oooo… yooo Kiberaaa
  Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
  Aaaa Ngulupaaa Ngulupaaa
  Aaaaa Ngulupaaa Ngulupaaaa
  Aaaa Ngulupaaa Ngulupaaa
  Ngulupaaa Ngulupaaa
  Ngulupaaa Ngulupaaaa
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibwacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Oooo…yoooh Kiberaa
  Kiberaa wee bwana Kiberaaa
  Ooo… yeeeh Kiberaaa
  Kiberaa wacha wee Kiberaaa
  Oooo… yooo Kiberaaa
  Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Oooo…yoooh
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Oooo…yoooh Kiberaa
  Kiberaa wee bwana Kiberaaa
  Ooo… yeeeh Kiberaaa
  Kiberaa wacha wee Kiberaaa
  Oooo… yooo Kiberaaa
  Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
  Kiberaa
  Kiberaa wee bwana Kiberaaa
  Ooo… yeeeh Kiberaaa
  Kiberaa wacha wee Kiberaaa
  Oooo… yooo Kiberaaa
  Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa
  Ooooo..  yeee Kiberaa
  Kibera wacha weee Kiberaaa  aaaah!
  Oooo…yoooh Kiberaa
  Kiberaa wee bwana Kiberaaa
  Ooo… yeeeh Kiberaaa
  Kiberaa wacha wee Kiberaaa
  Oooo… yooo Kiberaaa
  Kiberaa weee bwana Kiberaaaaa

  (IMEANDALIWA NA ALLY LITYAWI)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIBERA ACHA CHUKI YA KASONGO MPINDA NA MK GROUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top