• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  JELA YAMNG'ANG'ANIA MBAYA WA MUAMBA


  Liam Stacey kulia

  MWANAFUNZI ameshindwa rufaa yake jana kupinga huku ya kifungo cha kumkashifu kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba kwenye Twitter baada ya kuanguka na kupoteza fahamu kwa matatizo ya moyo.
  Liam Stacey, mwenye umri wa miaka 21, anayesoma Chuo Kikuu cha Swansea, alihukumiwa kwa kitendo chake cha kibaguzi kwenye Tweeter kufuatia kuzimia kwa Muamba uwanjani.
  Ametupwa jela kwa siku 56, tangu Jumanne.
  Rufaa yake ilitupiliwa mbali na Jaji wa Mahakama Kuu ya Swansea, Wyn Williams ambaye alisema: Stacey “alidhamiria kusema alichosema na alidhamiria kusababisha madhara aliyoyafanya.”
  Mapigo ya moyo ya Muamba yalisimama kwa dakika 78 baada ya kuzimia kwenye Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham Machi 17, mwaka huu.
  Amepona, lakini bado yupo hospitali Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JELA YAMNG'ANG'ANIA MBAYA WA MUAMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top