• HABARI MPYA

    Thursday, March 29, 2012

    SIR FERGUSON: HATA SISI TULINYIMWA PENALTI NA FULHAM


    Sir Alex Ferguson

    KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson leo amejibu mapigo ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, Manchester City kwamba mabingwa hao watetezi wanabebwa na marefa.
    Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Soka wa Manchester City, Patrick Vieira alinukuliwa kwa mapana marefu akisema kwamba United na klabu  nyingine kubwa Ulaya zinabebwa na marefa hasa katika mechi za nyumbani.
    Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal na City alitolea mfano United ilivyooepuka adhabu ya penalti, licha ya Michael Carrick kumchezea rafu Danny Murphy dakika za mwishoni Mashetani Wekundu wakishinda 1-0 dhidi ya Fulham Jumatatu.
    Baadaye City ilisema maneno ya Vieira yalikuwa yak wake mwenyewe – lakini Ferguson hakuona sababu ya kuyapuuza katika maelezo yake leo wakati mbio za ubingwa zinaelekea kileleni.
    Ferguson alisema United pia walitakiwa kupata penalti Jumatatu dhidi ya Fulham, akisema kwamba maamuzi kama hayo hata na wao wanakutana nayo.
    "Nafikiri tulitakiwa kupewa penalti Jumatatu usiku," alisema Ferguson.
    "Lakini usitarajie kupata kama hiyo, wakati mchezaji wa pembeni anatia krosi na mchezaji anaunawa mpira kwa bahati mbaya. Tungepeta penalti, lakini hatukutarajia, niwe mkweli kwao,”alisema.
    "Nafikiria hilo kulingana na nafasi ya refa, naweza kuona kwa nini refa hakutoa penalti wakati Danny Murphy alipoangushwea kwenye eneo letu la hatari, kwa sababu mpira ulikuwa unaelekea pembeni wakati Michael Carrick anakwenda kumkabili.
    "Kulingana na nafasi, haikuwa sahihi, lakini yalikuwa malalamiko mazuri.
    "Lakini pia City wangepata penalti dhidi ya Stoke, kama kila mtu alivyoona, wakati Gareth Barry alipomkabili Glenn Whelan. Hivyo hayo unakutana nayo hapa na kule.
    "Tulikumbana na uamuzi wa utata Old Trafford, wakati Newcastle walipopewa penalti. Tottenham wanaweza kulalamika hivyo pia wakati Balotelli alipoachwa uwanjani hadi akafunga bao la ushindi katika ushindi wa City 3-2, ingawa alistahili kutolewa kwa kadi nyekundu..
    Ferguson pia alitoa wasiwasi kwamba kipa Anders Lidegaard hatacheza tena msimu huu baada ya kuumia mazoezini, akisema kwamba anaendelea vizuri na maumivu yake ya kifundo cha mguu.
    Kocha huyo wa United pia amempata tena beki Rio Ferdinand aliyekuwa majeruhi kuelekea mechi ya Jumatatu ugenini dhidi ya Blackburn, na sasa majeruhi wake pekee ni Nani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIR FERGUSON: HATA SISI TULINYIMWA PENALTI NA FULHAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top