• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  DEMU AMPONZA MARADONA, MWENYEWE AWAKA KINOMA


  Maradona

  GWIJI wa soka wa Argentina, Diego Maradona amekerwa na mashabiki waliowashambulia wake na mahawara wa wachezaji baada ya vurugu za jana.
  Timu ya Maradona, Al Wasl ilifungwa 2-0 na Al Shabab katika Ligi ya UAE na kutokana na vurugu hizo ilibidi wake  na mahawara wa wachezaji wasindikizwe kutoka kwenye Uwanja wa Al Mamzar.
  Vurugu zilianza baada ya Ciel, mshambuliaji wa Kibrazil aliyefunga moja ya mabao, kufanyiwa jambo na mashabiki wa Maradona.
  Mashabiki wa Al Shabab walijibu mapigo wakielekeza kwa mpenzi wa Maradona, Veronica Ojeda na hawara wa mchezaji wa Al Wasl, Juan Mercier.
  Wakati wake na mahawara wakisindikizwa kwenye gari zao, hawara wa Mercier aliteleza na kuanguka kwenye ngazi.
  "Watu wengine ni waoga. Wanashambulia tu wanawake na hawana jeuri ya kuwafuata wanaume," alisema Maradona.
  "Hii ni mara ya kwanza ninakerwa na mashabiki. Kama wana hasira na mimi, wanatakiwa kujua nimefanya hivi (kupanda jukwaani) kwa ajili ya mke wangu, kwa sababu kuna mtu alikuw aanaita jina lake. Hawatakiwi kuwa na hasira na mimi, wawakasirikie watu waliofanya vile. Ni Waoga, si mashabiki halisi."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DEMU AMPONZA MARADONA, MWENYEWE AWAKA KINOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top