• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 26, 2012

  MUAMBA SASA ANAKULA, ANAACHA KITANDA

  Muamba
  KIUNGO wa Bolton Wanderers, Fabrice Muamba mwenye asili ya DRC, anaendelea vizuri na hali yake sasa inaridhisha, dokta amesema leo.
  Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 bado yupo kwenye cha wagongwa wenye uangalizi maalum katika hospitali ya London Chest alikolazwa tangu aanguke na kupoteza fahamu kwenye ya Robo Fainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspur Machi 17, mwaka huu.
  Taarifa ya pamoja iliyotolewa na hospitali hiyo na Bolton ilisema: "Fabrice Muamba bado yupo chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum katika hospitali ya London Chest, ambako hali yake ni mbaya, lakini yuko vizuri.
  "Anaendelea kuimarika katika kupata unafuu. Mwishoni mwa wiki alikuwa tayari anaweza kukaa mbali na kitanda kwa muda mfupi, kuangalia Televisheni na ameanza kula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MUAMBA SASA ANAKULA, ANAACHA KITANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top