• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  MTIMANYONGO WA WENGER KWA AC MILAN


  Wenger
  KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anafikiri C Milan haina nafasi ya kubeba ndoo ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
  "Kila mmoja anaiangalia Milan kwa heshima, lakini nafikiri hawana nafasi ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa," alisema Wenger.
  Mabingwa hao wa Serie A waliingia Robo Fainali baada ya kuitoa Arsenal kwa jumla ya mabao 4-3, mechi ya marudiano wakifungwa 3-0 Uwanja wa Emirates.
  Akizungumza saa chache kabla ya mechi kati ya AC Milan na Barcelona, Wenger alisema The Rossoneri wana safari ndefu kufikia kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.
  "Naifahamu Milan vizuri sana: wanacheza vizuri sana kwa ujumla, kitimu, lakini sifikiri wana uwezo wa kutwaa Kombe," alisema Wenger.
  "Wana udhaifu fulani, wana wachezaji wenye uwezo kama Zlatan Ibrahimovic. Robinho pia anaweza kuwa hatari sana katika ushambuliaji, lakini 'Ibra' anaweza kufunga mabao mengi akiamka vizuri."
  Alisema: "Milan wanajua cha kufanya ili washinde San Siro: Nafikiri hali ya Uwanja wao imeimarika, kwa sababu ilikuwa balaa dhiti yetu!"
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIMANYONGO WA WENGER KWA AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top