• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  MANCINI HANA IMANI NA BALOTELLI


  Bakitelli kulia na Mancini kushoto

  KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema katika vita kali ya ubingwa wa Ligi Kuu England, hamuamini Mario Balotelli.
  Kocha huyo Mtaliano, ambaye mfungaji wake bora Sergio Aguero ameumia mguu wiki hii, anakabiliwa na tatizo la washambuliaji kwani Edin Dzeko ndiye pekee aliyefunga mabao mawili katika mechi 17 zilizopita na Carlos Tevez ndio kwanza anarejea taratibu katika kiwango chake baada ya miezi mitatu ya kuwa likizo ya kujitakia kwao Argentina.
  Na mzigo huo unamuangukia Balotelli, pamoja na hayo Mancini hana uhakika kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anaweza kuaminiwa katika patashika ngumu ya mbio za ubingwa.
  "Simuamini Mario, lakini yupo hivi. Sifikiri kama yeyote anaweza kumuamini Mario," aliwaambia waandishi wa Habari. "Anaweza kufunga mabao mawili kwa urahisi kesho au katika mchezo mwingine na Arsenal. Lakini hatuwezi kumuamini."
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 hana shaka na uwezo wa mchezaji huyo wa zamani wa Inter, lakini swali ni juu ya kiwango mchake katika mechi za karibuni tangu amtoe nje kipindi cha pili mchezo katika wa City na Chelsea.
  "Ni mchezaji babu kubwa, anaweza kufanya kitu chochote mchezoni. Anaweza kufunga mabao matatu, lakini pia anaweza kupewa kadi nyekundu.
  "Ni kazi yake, anatakiwa kufanya kazi, anatakiwa kupumzika, lakini ni mdogo. Ninatumaini anaweza kufunga mabao matano au sita muhimu katika mechi nane zilizobaki.
  "Nilistaajabishwa na kiwango chake katika mechi na Chelsea, lakini si dhidi ya Stoke," alisema.
  Wawili hao walipigwa picha pamoja mapema wiki hii wakibishana, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Sampdoria alipuuza madai hayo.
  alisema: “Nilizungumza naye kwenye mazoezi kwa sababu nilikuwa namfafanulia kitu fulani uwanjani, ni hivyo tu.”
  Lakini kulikuwa kuna matatizo zaidi kwa Mancini wiki hii, wakati Balotelli aliporejea Milan katika siku zake mbili za mapumziko.
  Nyota huyo mzaliwa wa Sicily, alivamia Mkutano na Waandishi wa Habari wa kumtambulisha kocha mpya wa Inter kumsalimia kocha huyo Andrea Stramaccioni, ambaye amechukua nafasi ya Claudio Ranieri na kusabab isha usumbufu.
  Pamoja na hayo, Mancini anatumainin kwamba mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 20 anaweza kutumia muda wake mwingi kukua taratibu.
  "Siwezi kumchukua na kumfungia nyumbani kwake kwa siku mbili! Dhahiri wakati utafika atakapokuwa anaelewa nini anatakiwa kufanya anapopewa mapumziko ya siku mbili.
  "Natumaini anakua, kwa sababu anatakiwa kujirekebisha."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANCINI HANA IMANI NA BALOTELLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top