• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  KUZIONA SIMBA NA LYON BUKU TATU, KWA VIBOSILE 10,000 HADI 15,000E


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetaja viingilio vya mechi kati ya African Lyon na Simba SC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambavyo ni Sh. 3,000 kwa viti vya kijani na bluu, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 15,000.
  Yanga na Simba ni miongoni mwa timu nne zitakazokuwa viwanjani kesho kusaka pointi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo iko katika raundi ya 22.
  Yanga itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga  hiyo ikiwa mechi namba 148, ambayo itachezeshwa na refa Rashid Msangi wa Dodoma, atakayesaidiwa na Rashid Lwena (Ruvuma) na Issa Malimali (Ruvuma).
  Refa Amon Paul wa Musoma ndiye atakayechezesha mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Jumapili kutakuwa na mechi nyingine ya VPL kati ya Azam na Ruvu JKT itakayochezwa Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam ambayo kiingilio chake kitakuwa sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu.
  Hii ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KUZIONA SIMBA NA LYON BUKU TATU, KWA VIBOSILE 10,000 HADI 15,000E Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top