• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  OZIL AAPA KUFIA REAL


  Ozile

  KIUNGO wa Real Madrid, Mesut Ozil amesema alikuwa ana nafasi ya kujiunga na Inter Milan baada ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010, lakini akaamua kwenda Santiago Bernabeu.
  Sasa mambo yakiwa yamemnyookea Hispania, amesema anapenda kucheza Los Blancos hadi anastaafu.
  Gazeti la Sport-Bild limeripoti kuwa kocha wa zamani wa Inter Milan, Jose Mourinho kwanza alitaka kumsajili Ozil ahamie Serie A mwaka 2009, lakini akachelewa kuwahi dirisha la usajili.
  The Nerazzurri tena wakajaribu kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Werder Bremen kwa dau la Euro Milioni 25 kuimarisha safu ya kiungo katika kushambulia, lakini bahati mbaya
  Ozil akili yake ilikuwa kuhamia Madrid, alikohamia kwa dau la Euro Milioni 15 kuungana na Mourinho.
  "Ni kweli kwamba 2010 nilipata ofa kutoka klabu kibao kubwa Ulaya. Ikiwemo Inter. Lakini uamuzi wa kwenda Real ulikuwa sahihi.
  Ni klabu bora duniani, na ningependa kumalizia soka yangu hapa," alisema Ozil.
  "Nina miaka 23 tu, sitakuwa kwenye kiwango cha juu kwa muda mrefu. Hata niwe bora aje. Akili yangu yote ni Madrid na timu ya taifa, kwa sababu tunaweza kuweka historia mwaka huu.
  "Sisi [Real] tunaweza kutwaa La Liga na Ligi ya Mabingwa, na Euro nikiwa na Ujerumani."
  Nyota huyo wa Madrid alizungumzia pia kiwango cha mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi na hakuwa na cha zaidi ispokuwa kumtukuza Muargentina huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OZIL AAPA KUFIA REAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top