• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  ALGERIA MABINGWA U-17 KASKAZINI


  TIMU ya taifa ya Algeria imetwaa ubingwa wa Afrika Kaskazini kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, (UNAF) iliyomalizika mjini Kalaa Kebira, Tunisia wiki iliyopita.
  Junior Desert Foxes walitwaa taji hilo baada ya kutoa sare na wenyeji Tunisia kwenye michuano hiyo iliyoanza Machi 20 hadi 24.
  Algeria ilivuna pointi nyingi zaidi kwenye michuano hiyo iliyochezwa kwa mtindo wa mzunguko, Mauritania ikiwa timu nyingine iliyoshiriki.
  Algeria, washindi wa michuano iliyopita, walimaliza wakiwa na pointi nne, Mauritania tatu na Tunisia pointi moja.
  Wakati huo huo: Michuano ijayo ya UNAF U-17 itafanyika Dar El-Beida kuanzia Machi 27 hadi 30, washiriki wakiwa wenyeji Algeria, Mauritania, Morocco na Tunisia.

  MATOKEO UNAF U-17:
  Siku ya kwanza:
  Algeria 2-0 Mauritania
  Siku ya Pili
  Tunisia 1-2 Mauritania
  Siku ya Tatu
  Algeria 0-0 Tunisia

  MSIMAMO WAKE:
                         P   W   D   L   GF  GA  GD  Pts
  Algeria             2   1    1   0    2    0   +2    4
  Mauritania        2   1    0   1    2    3   -1     3
  Tunisia             2   0    1   1    1    2   -1     1
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALGERIA MABINGWA U-17 KASKAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top