• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  AC MILAN KATIKA MZITO KABLA YA SAFARI YA CAMP NOU


  WAKIWA kwenye kiwango kizuri, Catania hakika wanaitia presha vinara wa Serie A, AC Milan.
  Kocha Vincenzo Montella atawakosa beki Alessandro Potenza na kiungo Marco Biagianti kwa sababu ni majeruhi, lakini beki wa pembeni Marco Motta yupo kikosini tena licha ya Pablo Barrientos kupewa nafasi kubwa ya kuanza kama kiungo wa kulia.
  Kiungo mchezeshaji, Fracesco Lodi, anaweza kuongoza timu hiyo katika dimba la kati akiwatengenezea nafasi za kufunga Alejandro Gomez na Gonzalo Bergessio.
  Ikionekana kuwa na safu imara ya ulinzi baada ya kuikomalia Barcelona kwa sare ya 0-0 katika Ligi ya Mabingwa, Milan ina makovu kadhaa.
  Kiungo Sulley Muntari na beki wa kushoto Djamel Mesbah wanatumikia adhabu. Mark van Bommel atakuwapo tena baada ya kumaliza adhabu, lakini kuwepo kwa mkongwe Alessandro Nesta, anaweza kupumzishwa kwa ajili ya mechi ya marudiano na Barca Jumanne.
  Beki wa kati Thiago Silva anaendelea kuuguza maumivu yake baada kwenye mechi ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Roma na kwa manaa hiyo, Gianluca Zambrotta na Daniele Bonera kwa mara nyingine wataanza kwenye kikosi cha kwanza, licha ya kupona kwa Ignazio Abate.
  Wakati huo huo: mshambuliaji Maxi Lopez anaweza kucheza dhidi ya timu hiyo aliyoikimbia majira ya baridi msimu huu kuhamia San Siro, lakini inaonekana anaweza akaanzia benchi akiwapisha Zlatan Ibrahimovic na Stephan El Shaarawy.

  JE WAJUA?
  Catania imefungwa mechi moja tu katika mechi zake 10 zilizopita, 3-1 dhidi ya Juventus Februari 18 mjini Turin.
  The Sicilians wamefungwa mechi mbili tu Uwanja wa Angelo Massimino msimu huu na sasa wanashika nafasi ya saba katika Serie A.
  Catania ilifungwa 4-0  na The Rossoneri Novemba, mwaka jana Uwanja wa San Siro.
  AC Milan imeshinda mechi zake zote nne zilizopita Serie A, huku Ibrahimovic akifunga mabao saba katika kipindi hicho.
  Vijana wa Massimiliano Allegri, wameshinda mechi 10 ugenini katika Serie A msimu huu, ikiwa ni mechi nyingi kuliko timu zote msimu huu.
  Ni timu yenye wachezaji wengi waliofunga mabao, ikiwa wachezaji wake 17 tofauti wameifungia mabao Milan msimu huu.

  Vikosi;
  CATANIA: Carrizo, Belluschi, Legrottaglie, Spolli, Barrientos, Izco, Lodi, Almiron, Marchese, Bergessio na Gomez.
  AC MILAN: Abbiati, Zambrotta, Bonera, Mexes, Antonini, Aquilani, Ambrosini, Nocerino, Boateng
  Ibrahimovic na El Shaarawy.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AC MILAN KATIKA MZITO KABLA YA SAFARI YA CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top