• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  CHAMBERLAIN KUULA ARSENAL


  Chamberlain

  NYOTA wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain anaweza kujikuta anapata mshahara wa pauni 50,000 mwishoni mwa msimu, kutokana na mpango mpya wa kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger
  Licha ya kwanza Robin van Persie na Theo Walcott wataingia kwenye mazungumzo baada ya msimu, lakini pia suala la kinda huyo wa umri wa miaka 18, Oxlade-Chamberlain litajadiliwa.
  Kuhusu winga huyo ambaye msimu uliopita alichezea Southampton, Wenger inasemekana amevutiwa mno na kiungo huyo na anamuandalia mkataba mnono.
  Inafikiriwa kwamba atapata mshahara mara mbili ya anaoupata sasa, pauni 25,000 kwa wiki.
  Pia kuna tetesi kwamba The Gunners watatangaza kumsajili nyota wa Ujerumani Lukas Poldolski siku chache zijazo kwa dau la pauni Milioni 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHAMBERLAIN KUULA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top