• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  TERRY VENABLES ARUDI KAZINI ENGLAND


  Terry Venables

  KOCHA wa zamani wa England, Terry Venables amerejea kwenye soka baada ya miaka minne na nusu ya kuachana nayo, kwa kujiunga na Wembley FC, timu inayocheza daraja la tisa la soka ya England.
  Babu huyo wa miaka 69, Venables, ambaye aliiongoza England kufika Nuau Fainali ya Euro 1996, ametajwa kuwa Mshauri mpya wa Ufundi wa timu hiyo isiyoshiriki ligi, ambayo ina mashabiki wasiozifi 100.
  Kwa mara ya mwisho, Venables alikuwa Msaidizi wa kocha wa England, Steve McClaren, kabla ya wote wawili kutimuliwa Novemba 2007, baada ya timu hiyo kukosa tiketi ya Euro 2008.
  Wembley FC imemudu kumchukua Venables baada ya kupata udhamini wa Budweiser, ambao pia wapo katika mwaka wa kwanza katika miaka mitatu ya udhamini wa Kombe la FA England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TERRY VENABLES ARUDI KAZINI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top