• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  MGOSI AWAVAA TP MAZEMBE


  Mgosi

  MUSSA Hassan Mgosi, anatarajiwa kuiongoza Daring Club Motema katika mechi kali ya Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi ya Tout Puissant Mazembe Aprili 1, mwaka huu.
  Hata hivyo, siku hiyo Mussa hatamshuhudia mshambuliaji mwenzake wa zamani wa Simba SC, Mbwana Ally Samatta ambaye kwa sasa ni majeruhi.
  Lakini Mussa anaweza kupishana pishana uwanjani na kiungo Mganda, Patrick Ochan ambaye alikuwa naye Simba SC mwaka jana kabla ya wote kuhamia DRC.
  Katika mechi hiyo itakauopigwa kwenye Uwanja wa Stade Kibassa Maliba, Lubumbashi- Mussa pia anaweza kukutana uwanjani na Mtanzania mwenzake, Thomas Ulimwengu anayechezea TPM, ingawa bado si mchezaji wa kudumu kikosi cha kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MGOSI AWAVAA TP MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top