• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  SAMATTA KUTIBIWA AFRIKA KUSINI


  Samatta

  KLABU ya TP Mazembe imesema maumivu ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta si ya kutisha lakini wamepanga kumpeleka Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi.  
  Samatta ambaye ataikosa mechi kali dhidi ya DC Motemba Pembe Aprili 1, mwaka huu katika Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), aliuamia bega kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos nchini Zambia.
  Siku hiyo, Samatta au ‘Samagoal’ kama wamuitavyo mashabiki wa TPM alifunga bao timu yake ikitoa sare ya 1-1 na kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele.
  Tovuti ya TPM imesema Samatta yuko chini ya uangalizi makini wa wataalamu wa tiba wa klabu hiyo na amekuwa akiupa mazoezi kidogo mkono wake.
  Samatta amekuwa akihudhuria kliniki ya TPM kila asubuhi na jioni pamoja na kutibiwa, lakini pia akijengwa kisaikolojia.
  Mchezaji mwingine wa Mazembe aliyekuwa anasumbuliwa na nyama kwa wiki mbili, beki Hichani Himonde amepona na ameanza mazoezi.
  Samatta ataikosa pia mechi ya marudiano na Power Dynamos Aprili 8, mwaka huu, Stade Kibassa Maliba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA KUTIBIWA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top