• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  PICHA YA KWANZA YA MUAMBA AKITABASAMU TANGU AFE KWA MUDA

  HII ni picha ya kwanza ya tabasamu ya Fabrice Muamba tangu azimie na kupoteza kufahamu, ambayo imewekwa kwenye Twitter na mpenzi wake.
  Nyota huyo aliyezimia uwanjani siku 13 zilizopita katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham, alipigwa picha hii akiwa amekaa hospitali.
  Swahiba wake Shauna Magunda, mwenye umri wa miaka 27, alisema: "Fab alinitaka mimi nikaibandike picha hii kwa ajili yenu wote na pia kuwashukuru kwa sapoti kubwa mliompa."
  Picha hiyo imewekwa kwenye kurasa maalum za wapenzi hao, ikimuonyesha nyota huyo wa Bolton anavyoendelea vizuri.
  Dokta alisema; kitaalamu ‘alikuwa amekufa’ kwa dakika 78 baada ya kuzimia kwenye Uwanja wa White Hart Lane Machi 17.
  Alihitaji shocks 15 ili mapigo ya moyo wake kuanza kutembea tena akiwa njiani kupelekwa hospitali ya London Chest, Bethnal Green.
  Kisha Muamba alikaa hospitali hapo siku kadhaa akiwa katika hali mbaya, lakini hatimaye kwa dua za jamii ya soka amepona.
  Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuweza kutembeza mikono yake na miguu na kuitambua familia yake.
  Neno la kwanza la Muamba tangu apone lilikuwa ni kuhusu mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, Joshua.
  Alianza kutia matumaini Machi 21.
  Kwa muda wote amekuwa akihudumiwa pia kwa umakini na familia yake, akiwemo mpenzi wake Shauna na wazazi wake Marcel na Gertrude.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PICHA YA KWANZA YA MUAMBA AKITABASAMU TANGU AFE KWA MUDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top