• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  MABILIONEA WATANO WENYE FEDHA CHAFU LAKINI HAWAJAOA

  Alejandro Santo Domingo
  Akiwa ana umri wa miaka 35, tayari ana utajiri wa dola za Kimarekani Bilioni 9.5.  Raia huyo wa Colombia, ambaye alihitimu masomo yake katika chuo cha Harvard mwaka 1999, sehemu kubwa ya utajiri wake amerithi kwa marehemu baba yake. Mkazi huyo wa Manhattan anahusishwa na skendo za kutembea na vimwana wakali kama Amanda Hearst na mwanamitindo Julie Henderson, ambaye kwa sasa anaishi naye.
  Yoshikazu Tanaka
  Akiwa ana umri wa miaka 35, ana utajiri wa dola za KImarekani Bilioni 3.5.
  Mtu huyo kutoka bara la Asia ni mwanzilishi na CEO kampuni ya game za mitandao inayoongoza Japan, Gree. Kampuni hiyo ilichukua game ya mtandao ya Marekani, OpenFeint mwaka jana.
  Robert Pera
  Akiwa ana umri wa miaka 34, ana utajiri wenye thamani ya dola za KImarekani Bilioni 1.5.
  Mtaalamu huyo wa programua ya kompyuta ya Apple, ambaye aliibuka mwaka 2005 na kuwa bilionea Oktoba mwaka 2011 wakati program yake ya Ubiquiti Networks iliposambaa, hakuna ajabu hadi sasa hana mke. Anapiga kazi, anacheza hoops na anaishi simpo tu katika nyumba yenye fenicha za kawaida na chumba kimoja tu cha kulala huko San Jose.
  Eduardo Saverin
  Akiwa ana umri wa miaka 30, ana utajiri wenye thmani ya dola za KImarekani Bilioni 2. Mwanzishaji huyo mshiriki wa Facebook, Eduardo Saverin, ambaye anatimiza miaka 30 akiwa hana mke, alizaliwa Brazil, akahirimu masomo yake Chuo Kikuu cha Harvard na sasa anaishi Singapore.
  Albert von Thurn und Taxis
  Akiwa ana umri wa miaka 28, ana utajiri wenye thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 1.5.
  Bilionea huyo mdogo, lakini bado hajaoa na Albert von Thurn und Taxis bado anaishi familia yake ya wakimbiza magari huko Ujerumani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MABILIONEA WATANO WENYE FEDHA CHAFU LAKINI HAWAJAOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top