• HABARI MPYA

    Tuesday, March 27, 2012

    SIMBA KAMBI MISRI, MKAKATI MZITO KUMNG'OA MWARABU HUU HAPA

    
    Kikosi cha Simba
    OLIVER ALBERT (gazeti la Mwanaspoti)
    BAADA ya kujiwekea mtaji wa mabao 2-0, Simba itakwenda Misri kusaka dawa ya kuing'oa Entente Setif ya Algeria kwenye mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa katika mji wa Setif nchini humo Aprili 6.
    Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Simba itaondoka Jumatatu ijayo kuelekea Cairo, ambako itaweka kambi kwa siku mbili na kuelekea Algeria.
    Kiongozi mmoja wa klabu hiyo aliitonya Mwanaspoti kuwa walikuwa wanahaha jana Jumatatu ili kuomba nafasi kwenye Shirika la Ndege la Misri kwa ajili ya safari hiyo.
    Simba, baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0, imeamua kwenda Misri ambayo ni nchi ya Afrika Kaskazini kama Algeria, ili kujizoeza na hali ya hewa kabla ya mechi ya marudiano.
    Vipimo vya hali ya hewa ya Algeria ni kwenye nyuzi joto 16 wakati ile ya Cairo ni kwenye nyuzi joto 17.
    Simba, ambayo imeandaa bajeti ya Sh 200 milioni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, imepanga kufanya mazoezi ya siku mbili nchini Misri kabla ya kwenda Algeria ambako itarudiana na Entente mjini Setif. Hata hivyo, haikujulikana mara moja kama watacheza mechi za kirafiki.
    Ili kusonga mbele, Simba inatakiwa kuifunga Entente Setif kwa idadi yoyote ya mabao, sare au kufungwa chini ya bao moja.

    Historia yajirudia
    Simba imeamua kutorudia makosa ya Yanga, ambao walikwenda Misri bila kujipanga na matokeo yake wakatolewa na Zamalek kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.
    Timu hiyo ilizitoa timu za Afrika Kaskazini mara zote ilipoweka kambi katika maeneo yanayofanana na huko kabla ya kuvaana.
    Mwaka 1993, iliweka kambi yake katika mji wa Nice, Ufaransa kabla ya kurudiana na El-Harrach katika mechi ya Kombe la CAF nchini Algeria.
    Simba ilikwenda huko baada ya kuwa imeshinda mchezo wa kwanza 3-0 jijini Dar es Salaam na baada ya kambi ile ilifungwa 2-0 nchini Algeria na kupita kwa jumla ya mabao 3-2.
    Ilifika fainali ya mashindano hayo katika mwaka huo ingawa ilifungwa na Stella Abidjan ya Ivory Coast 2-0 mjini Dar es Salaam.
    Pia mwaka 2003 ilipoivua Zamalek ubingwa wa Afrika, iliweka kambi yake nchini Oman. Iliitoa timu hiyo kwa penalti jijini Cairo, Misri.

    Ushauri wa Milovan
    Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic ndiye ameshauri viongozi wa Simba wafike siku tatu kabla ya mechi hiyo nchini Algeria ili kuzowea hali ya hewa kuepuka isiwaathiri wachezaji wakacheza chini ya kiwango.
    �Kule hivi sasa ni baridi sana, hivyo itabidi tuwahi kufika ili kwenda sambamba na hali ya hewa, tukizowea kila kitu kitakwenda vizuri,� alisema Cirkovic baada ya mchezo wa juzi Jumapili.

    Dosari ya mchezo wa kwanza
    Pamoja na ushindi wa 2-0, kocha Milovan Cirkovic ametahadharisha kuwa timu yake ina kibarua kigumu kwenye mchezo wa marudiano.
    Cirkovic alieleza kuwa anapaswa kufanya marekebisho kwenye safu ya ushambuliaji kabla ya mchezo wa Algeria.
    Safu ya ushambuliaji ya Simba iliyoongoza na Emmanuel Okwi iliikosesha timu hiyo mabao mengi.
    Okwi, ambaye ndiye mfungaji tegemeo kwenye timu hiyo akiwa na mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara, alikosa mabao matano ya wazi. Felix Sunzu alikosa mabao matatu.
    �Nawapongeza wachezaji wangu kwa kupambana na kuweza kushinda katika mechi ngumu, nimeona makosa kadhaa hasa safu ya ushambuliaji.
    "Tunatakiwa kufanya mazoezi ya uhakika katika siku 10 kabla ya mechi ya marudiano ili tuweze kufunga mabao ugenini.
    �Ninachoshukuru hawajaweza kupata goli kwetu, hivyo inabidi tukienda kule tupambane kwa kiwango kikubwa,
    tuongeze kasi mara mbili ya hapa ili tupate ushindi mwingine, maana najua kwao watatumia kila mbinu ili kutumaliza, lakini hatuna budi kukabiliana nayo ili twende raundi nyingine,� alisema Cirkovic, raia wa Serbia.

    Mapokezi ya Simba
    Kiongozi mmoja wa Simba, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake aliitonya Mwanaspoti kuwa Watanzania wanaoishi Algeria wameandaa mapokezi makubwa kwa ajili ya timu hiyo nchini humo.
    Viongozi wa Watanzania wanaoishi katika nchi hiyo wamewahamasisha Waafrika wengine wanaoishi nchini humo ili kuishangilia timu hiyo itakapocheza mjini Setif.
    Alieleza kwamba wamewahamasisha mashabiki wapatao 500 kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wamejipanga kuishangilia timu hiyo.
    Mashabiki hao ndio waliisaidia Taifa Stars ilipokwenda huko mwaka 2010 na
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA KAMBI MISRI, MKAKATI MZITO KUMNG'OA MWARABU HUU HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top