• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  BEKI LA SENEGAL MIEZI MITATU KITANDANI

  Diawarra
  BEKI wa Olympique Marseille, Souleymane Diawara atakwenda kufanyiwa upasuaji wa goti zoezi ambalo litamfanya awe nje ya Uwanja kwa miezi sita, imesema klabu yake Ligi Kuu Ufaransa, Ligue 1 jana.
  Beki huyo wa kati wa Senegal, Diawara aliuamia vibaya goti lake la kulia hadi kutoa machozi Jumamosi, timu yake ikitoka 1-1  na Nice.
  “Atakwenda kufanyiwa upasuaji wiki ijayo. Atakuwa nje ya Uwanja kwa kiasi cha miezi sita,” ilisema Marseille katika tovuti yake.
  Diawara ataikosa sehemu yote ya msimu iliyobaki na atakuwa tayari kuanza tena kazi wakati msimu ujao unaanza Agosti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI LA SENEGAL MIEZI MITATU KITANDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top